Ehud Olmert
Mahakama moja nchini Israel imempa kifungo cha miaka
sita jela aliyekuwa waziri mkuu nchini Israel Ehud Olmert kwa kosa la
kupokea hongo.
Bwana Olmert alipatikana na hatia mwezi machi
katika kile kilichojulikana kama 'swala la eneo takatifu' ambapo hongo
ilitolewa ili kuharakisha ujenzi wa majumba ya kifahari mjini JerusalemKiongozi huyo alikuwa ameondolewa mashitaka katika kesi tofauti zilizokuwa zikimkabili.
Mashitaka yaliomkabili yalitekelezwa wakati Olmert alipokuwa meya wa mji wa Jerusalem na baadaye akiwa waziri wa serikali.
Ehud Olmert alimrithi Ariel Sharon kama waziri mkuu mnamo mwaka 2006 baada ya Sharon kuugua ugonjwa wa kiharusi.
Alijiuzulu mnamo mwaka 2008.