Michele Obama emejiunga na kampeni hii kutaka kuachiliwa kwa wasichana wa Nigeria
Wiki tatu tangu wasichana zaidi ya miambili kutekwa nyara na Boko Haram
nchini Nigeria, Jana ndio Marekani ilitangaza kutuma kikosi maalum
kusaidia Nigeria kuwatafuta wasichana hao
Je kimya hiki kilichukua muda mrefu kwa nini, jee kujihusisha kwa Marekani wakati huu kutasaidia hali?
Matukio machache yametendeka huku dunia nzima ikichukua muda kujibu
mfano ikiwa hii taarifa ya kutekwa kwa wasichana wa Nigeria kutoka
katika shule yao ya mabweni Kaskazini mwa Nigeria.
Maandamano yamefanyika mjini New York, Los Angeles na London,wakati
ujumbe mwingi kupitia kwenye mitandao ya kijamii ikitolewa sio tu kwa
Boko Haram bali pia kwa serikali ya Nigeria kwa kuonekana kama isioguswa
na tukio hilo.
Mnamo siku ya Jumatano, mke wa Rais wa Marekani
Michelle Obama alituma ujumbe kwa Twitter uliosema 'BringBackOurGirls'
yaani ''#Turudishieni wasichana wetu'' kuongeza sauti yake kwa kampeini
ambayo imewaka moto dunia nzima.
Ni wiki tatu tangu kutekwa nyara kwa wasichana wa Nigeria. Boko Haram imesema
itawauza wasichana hao
Hii ni kamepin iliyoanza nchini Nigeria kuwataka Boko Haram kuwaaachilia wasichana hao.
Mchango wake kwa kampeini hii umekuja siku moja
baada ya Marekani kutangaza kupeleka kikosi kusaidia Nigeria. Kikosi
hicho kitasaidia Nigeria kwa upande wa
uchunguzi, kuzungumza na wapiganajji kuwashawishi kuwaachilia wasichana na kuwasaidia waathiriwa.
Alipouliozwa kwa nini ilichukua mda mrefu,
waziri wa mambo ya kigeni John kerry alijibu kuwa Marekani ilikuwa
imejitolea kusaidia lakini serikali ya Nigeria ikawa haiko tayari kwa
hilo.
"tumekuwa tukishauriana tangu tukio hilo
kuripotiwa, lakini inaonekana serikali ya Nigeria ilikuwa na mikakati
yake, '' alisema Kerry.
Lakini jibu hilo halijawakomesha watu kuuliza,
kwa nini nchi za magharibi zimejikokota katika kusaidia Nigeria kama
vile, Ufaransa, Uingereza na Marekani? Hata hivyo licha ya malalamiko
haya msemaji wa serikali ya Uingereza amekanusha madai kuwa nchi hizo
zimechelewa kusaidia Nigeria.
Baadhi ya wachanganuzi wamefananisha kuchelewa
kwa mataifa hayo kusaidia Nigeria kinyume na ilivyokuwa wakati ndege ya
Malaysia MH370 ilipopotea huku mataifa mengi tu yakijitolea kusaidia
Malaysia.
Wakati mwingine bara la Afrika linaweza kuwa
giza kuu kwa mataifa ya Magharibi , lakini sio kwa wakati huu ambapo
msaada mkubwa unahitajika.
Thursday, 8 May 2014
Browse: Home
» Je Marekani imechelewa kusaidia Nigeria?
Je Marekani imechelewa kusaidia Nigeria?
Posted by mkachu | Tagged as:
Habari na U Chambuzi
HALI YA HEWA
TANGAZANASI
MTANDAO WA KIJAMII
ZILIZO SOMWA ZAIDI
-
eshi la Marekani limefanya shambulizi la makombora dhidi ya mtu anayeshukiwa kuwa mmoja wa viongozi wa al-Shabaab nchini Somalia. ...
-
Chama Cha Mapinduzi (CCM) party stalwart Rostam Aziz has earned USD 240 million (about Tsh. 384,000,000,000/-) from selling part of his st...
-
Wanaume wengi wanapofikia hatua ya kuoa si kwamba wanakurupuka tu na kuoa mwanamke yeyote mwenye sura nzuri, bali huchukua muda wao mw...
-
Kundi moja la wanawake walio na hisia za kimapenzi na mapadre wa kikatoliki wamemuandikia barua kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa F...
-
Madrasa hii ilianzishwa mnamo mwaka 2005 ikiwakama madrasa ya nyumbani ikiwa ndani ya jiji la Mwanza katika kito ngoji cha Bugando je...
-
Juhudi za serikali dhidi ya kundi hilo hazijaonekana kuzaa matunda Taarifa kutoka nchini Nigeria, zinasema kuwa mamia ya watu waliuawa...
-
Baadhi ya wanawake wengi wa hapa mjini wameanza kutumia style mpya ya kugundisha nywele aka wiving katika vichwa vyao kwa kutumia gu...
-
Marekani kusaidia kuwasaka wasichana waliotekwa na Boko Haram Serikali ya Nigeria inasema kuwa iko tayari kuzingatia mbinu zote zitakazo...
-
Baadhi hutengeza maji ya sharubati kwa kuichanganya na matunda Baadhi wanaamini kuwa Kondo la nyuma huwa na madini mengi ambayo hayapaswi...
-
Inspector Henry akiwasihi mahabusu hao wawili wanaotuhumiwa kwa kesi za mauaji, kuachia mlingoti wa Bendera ya Taifa na kurudi kwenye chum...
MITANDAO YA KIJAMII
TAFUTA HABARI ZILIZO SOMWA NYUMA
Pages
WALIO TEMBELEA
Powered by Blogger.
TANGAZA NASI
kwama Matangazo wasiliana nasi kupitia anuani zifuataz
Email:
mohamedwaziri295@gmail.com
mohamedwaziri21@yahoo.com
contact us:
0762118805
0658118804
info@islamicnews.blogspot.com
Wote mnakalibishwa
Email:
mohamedwaziri295@gmail.com
mohamedwaziri21@yahoo.com
contact us:
0762118805
0658118804
info@islamicnews.blogspot.com
Wote mnakalibishwa
Total Pageviews
3208
Labels
DOWNLOAD QASWIDA
islamic
islami news
Social Icons
islamic
Blog Archive
-
▼
2014
(48)
-
▼
May
(34)
- SIKIA LADHA ZA NYUMBAN HAPA
- JAMANI TUSEMEN WOTE KWAPAMOJA INA LILAHI WAINA ILA...
- Je Unazijua Tabia Za Mwanamke Wa Kuoa Au Huwa Watu...
- Diva Aweka Picha Mtandaoni Akiliwa Denda
- Tanzania yaibamiza Zimbabwe 1 - 0
- Wanafunzi wapinga kuongezwa karo Kenya
- TZ yapambana na Homa ya Dengue
- Pistorius kufanyiwa uchunguzi wa akili
- Wanawake waomba mapadre waoe
- Ehud Olmert jela kwa miaka sita
- UN yalaaani shambulizi Somalia
- Nigeria tayari 'kulegeza msimamo'
- ALBINO AUAWA, ACHUKULIWA VIUNGO VYAKE HUKO SIMIYU
- Njia za kula Kondo la Nyuma
- Je ulijua kama Kondo la Nyuma au 'Placenta' huliwa?
- Kwa Wale Wadada Wa Mjini Wanaopenda Kuvaa Mawigi K...
- Marekani yaanza kutumia makombora yenye madin ya y...
- ManCity wanukia ubingwa England
- Cameron:Waliotekwa Nigeria warejeshwe
- Mapigano yazuka upya Sudan Kusini
- Mradi wa reli mpya watiwa saini Nairobi
- Tazama Picha 10 Za Mahabusu Walioamua Kuvua Ngua N...
- Mfahamu Tajiri Namba Moja Hapa Tanzania Mwenye Mab...
- ANGALIA MWILI WA FIRAUN-LANA TULLAH
- Je Marekani imechelewa kusaidia Nigeria?
- INNA LLAHI WA INAILAIKA RAJIUN
- Mamia wauawa na Boko Haram Nigeria
- Wito wa kuwaokoa wasichana Nigeria
- Putin hataki kura ya maoni Ukraine sasa
- Kisanga cha mahabusu kuvua nguo TZ
- MARKAZ MISS BAHUL HUDA IMEANZISHWA MNAMO MWAKA 2005
- Vita vya ndugu kupiganiwa ugenini
- Nigeria kufunga Shule na Ofisi Jumatano
- Watatu wauawa kwa bomu Mombasa
-
▼
May
(34)
Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...