Tuesday, 13 May 2014

Je ulijua kama Kondo la Nyuma au 'Placenta' huliwa?

Posted by mkachu  |  Tagged as:

Baadhi ya wanawake wanakunywa maji ya Kondo la Nyuma saa chache baada ya kujifungua
Hugeuka kuwa uchafu pindi mama anapojifungua , sasa kwa nini baadhi ya wanawake wanaamua kula Kondo la nyuma au Placenta ikiwa mbichi ?
Kondo la Nyuma huwa ni sehemu ya mwili wa mama anapokuwa mjamzito, sehemu hiyo humsaidia mtoto kupata chakula na hewa kutoka kwa mama akiwa tumboni.

Pindi mama anapojifungua kazi ya Kondo la Nyuma huisha papo hapo na hivyo hutupwa , lakini sio kila mtu ana mtazamo huu.
Baadhi ya wanawake wanaamini kuwa madini yanayopitia kwa mkondo wa Nyuma hadi kwa mtoto ili kumuwezesha mtoto kukuwa huwa bado yanaweza kutumika na kwamba sio vizuri kuitupa.

Wanasema kuwa mama bado anaweza kupata madini muhimu wakati anapoendelea kupata nafuu baada ya kujifungua na pia anapoanza kuonyonyesha kwa kula Kondo la nyuma. 

Mama ale Kondo la Nyuma?'
Baadhi ya wanawake husaga kondo hilo na kunywa maji yake saa chache tu baada ya kujifungua, baadhi wanaihifadhi na kutengeza tembe ambazo wanameza na wengine wanaikata vipande vipande kwa kuweka chini ya ndimi zao.

Wanafanya hivyo kwa kuamini kuwa tembe hizo zinaweza kuwapa nguvu na pia kusaidia maziwa ya mama kuongezeka.
Kampuni moja nchini Uingereza inayotengeza biadhaa mbali mbali kutoka kwa Kondo la Nyuma, hulipisha watu kati ya pauni 150 au dola elfu kumi na saba kwa kila tembe na chini ya dola hamsini kwa maji ya kondo hilo linaposagwa.

Habari na U Chambuzi

    Author

    CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

    Subscribe to our Mailing List

    We'll never share your Email address.
    +255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com