Timu tatu za Hispania zimefanikiwa kucheza fainali mbili
tofauti za mashindano yenye hadhi ya juu barani Ulaya mwaka 2014.
Timu hizo mahasimu zimefikia hatua hiyo baada ya Real Madrid
kuwachabanga waliokuwa mabingwa watetezi wa kombe hilo
Bayern Munich ya
Ujerumani kwa jumla ya mabao 5-0. Real
Madrid ilipata ushindi wa bao 1-0
nyumbani, huku ugenini ikiisambaratisha Bayern magoli 4-0
Nayo Atletico Madrid baada ya kushindwa kuifunga Chelsea katika
uwanja wa nyumbani kwa kutoka suluhu ya 0-0, katika mchezo wa marudiano
wa nusu fainali katika uwanja wa Stanford Bridge jijini London, Chelsea
ilikiona cha moto kwa kuchabangwa magoli 3-1.
Wachezaji wa Atletico Madrid wakishangilia moja ya magoli yao
Kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1967, fainali za kombe la ligi ya mabingwa la UEFA zinafanyika mjini Lisbon.
Baadhi ya wachezaji wa Sevilla walioitoa Valencia
Sevilla imefuzu kucheza fainali hizo baada ya kuwatoa ndugu zao Valencia katika mchezo wa nusu fainali baada ya matokeo ya 3-3 lakini ikinufaika na goli la ugenini. Katika mchezo wa awali wa nusu fainali, Sevilla iliibuka na ushindi wa 2-0 katika uwanja wake wa nyumbani, lakini ikapata kipigo cha 3-1 ugenini na kufanya matokeo kuwa 3-3.