Friday, 24 January 2014

Syria yatishia kujiondoa Geneva

Posted by mkachu  |  Tagged as:

Waziri wa mambo ya nje wa Syria, Walid Muallem, ametoa tisho la kujiondoa kwenye mazungumzo ikiwa hakuna hatua zitakazokuwa zimefikiwa Jumamosi

 Mamilioni ya watu wameachwa bila makao kutokana na vita nchini Syria
 Waakilishi wa serikali ya Syria katika mazungumzo ya amani kati ya wanaharakati na serikali, wametishia kuondoka kwenye mazungumzo hayo ya amani ikiwa mazungumzo muhimu hayatakuwa yameanza ifikapo Jumamosi.

Waziri wa mambo ya nje wa Syria, Walid Muallem, ametoa tisho la kujiondoa kwenye mazungumzo baada ya kukutana na mjumbe maalum wa UN nchini Syria Lakhdar Brahimi.

Bwana Brahimi anatarajiwa kukutana na upande wa upinzani baadaye Ijumaa.
Duru zinasema kuwa mazungumzo yamekumbwa na changamoto hasa kwa kuwa pande zote mbili zina misimamo mikali.

Mgogoro wa kisiasa nchini Syria, umesababisha vifo vya watu 100,000 kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.
Ghasia hizo pia zimesababisha watu milioni 9.5 kutoroka makwao, na kusababisha hali mbaya ya kibinadamu ndani ya Syria na katika nchi jirani.
Hii ni siku ya tatu ya mazungumzo mjini Geneva lakini mkutano wa kwanza rasmi ambapo mazungumzo yanaanza.
Kulikuwa na matumaini ya mkutano wa ana kwa ana kati ya serikali na wanaharakati, lakini baadaye bwana Brahimi alifanya mazungumzo na kila upande.
Pande hizo zinalaumiana kwa changamoto hiyo.

Habari na U Chambuzi

    Author

    CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

    Subscribe to our Mailing List

    We'll never share your Email address.
    +255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com