Thursday, 8 May 2014

Mamia wauawa na Boko Haram Nigeria


 
Juhudi za serikali dhidi ya kundi hilo hazijaonekana kuzaa matunda

Taarifa kutoka nchini Nigeria, zinasema kuwa mamia ya watu waliuawa katika shambulizi lililofanywa na kundi la wapiganaji wa Boko Haram katika mpaka wa nchi hiyo na Cameroon siku ya Jumanne.

Katika mahojiano na BBC kiongozi mmoja wa eneo hilo, Ahmed Zanna, alisema kuwa washukiwa walivamia mji wa Gamboru Ngala, katika jimbo la Borno, na kuwaua takriban watu 300.

Inaarifiwa wapiganaji hao waliwafyatulia risasi watu kiholela katika soko kuu la eneo hilo.
Mwandishi wa BBC nchini Nigeria anasema ilikuwa vigumu kupata taarifa hizo mapema kwa sababu ya changamoto ya mawasiliano katika jimbo hilo hasa kwa sababu eneo hilo liko mbali sana.
Wakazi wa eneo hilo wanasema kuwa walipata zaidi ya maiti miamoja kutokana na shambulizi hilo.
Read more »

Wito wa kuwaokoa wasichana Nigeria

Read more »

Putin hataki kura ya maoni Ukraine sasa


Asema uchaguzi wa Urais uliopangwa kufanywa Mei 25, ni hatua inayofaa.

Katika hatua ambayo haikutarajiwa Rais wa Urusi, Vladimir Putin, ametoa wito kwa makundi yanayotaka kujitenga wanaounga mkono Urusi Kusini Mashariki mwa Ukraine waahirishe kura ya maoni ya Jumapili juu ya kutaka kujitenga kama hatua muhimu kuimarisha mashauriano ya amani kati ya makundi yanayozozana nchini humo.

Rais Putin alisema kuwa hatua hiyo itaimarisha mazingira ya kufanya mashauriano kati ya Serikali ya Ukraine na wale nchini wanaopendelea Urusi wanaotaka maeneo yao kujitenga na kuungana na Urusi.

Amesema kuwa uchaguzi wa Urais uliopangwa kufanywa Mei 25, ni hatua inayofaa.
Siku chache zilizopita Bwana Putin alitaja uwezekano wa kuwa na uchaguzi huo wa Urais kama upuzi mtupu. Lakini katika taarifa ya hivi sasa Bwana Putin amesema uchaguzi huo hautakuwa na maana iwapo raia wote wa Ukraine hawatahusishwa na kuwahakikishia jinsi haki zao zitakavyolindwa baada ya uchaguzi.
Vladmir Putin pia alidai kuwa Urusi imewaondoa wanajeshi wake kwenye mpaka wake na Ukraine.
Hata hivyo mataifa ya Magharibi yanatarajiwa kutoamini hakikisho hili hadi watakaposhuhudia kinachoendelea mpakani.
Mataifa hayo pia yanasubiri kuona iwapo taarifa ya Putin itapunguza uhasama miongoni mwa wananchi wa Ukraine.



Read more »

Wednesday, 7 May 2014

Kisanga cha mahabusu kuvua nguo TZ


Mahabusu wa Gereza Kuu la Mkoa wa Arusha, kaskazini mwa Tanzania, Jumanne walisababisha vurugu katika viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi mjini humo baada ya kuvua nguo na kugoma kushuka kwenye basi lililowachukua kwenda mahakamani wakipinga kitendo cha watuhumiwa wawili wa dawa za kulevya kuachiwa huru

Watuhumiwa wanaolalamikiwa ambao mashtaka yao yalibadilishwa mara mbili ili wapewe dhamana ni Dharam Patel na Nivan Patel wanaodaiwa kukamatwa na kete 173 za heroini na misokoto 300 ya bangi, Aprili,2014

Kwa mujibu wa watu waliokuwa katika eneo la mahakama hayo, mahabusu hao walikuwa wakipaza sauti kupinga madaraja(ubaguzi) miongoni mwa watuhumiwa, wenye uwezo kifedha na wasio nacho, hali ambayo imesababisha wengine kuachiwa na wengine kuendelea kusota magerezani kwa kisingizio cha "upelelezi haujakamilika
Mahabusu hao walisikika wakipaza sauti kutoka ndani ya basi: "Wenzetu hata mwezi haujaisha wanafutiwa kesi, jamani sisi tumekosa nini? Tunataka haki itendeke kwa wote" walisema.
Kuachiwa kwa watuhumiwa wanaolalamikiwa na mahabusu wenzao kunasemekana kumetokana na hatua ya Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Arusha kubadilisha hati ya mashitaka na hivyo kuwawezesha kupata dhamana.
Kamanda wa Kikosi cha Polisi cha Kuzuia Dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa ameliambia gazeti la Mwananchi kuwa ofisi yake haina taarifa za watuhumiwa hao kupewa dhamana lakini alisema kulikuwa na jaribio la kufanya hivyo.
Bwana Nzowa amesema baada ya kubainika njama hizo, ofisi yake ilipinga, akisema kuwa kosa la watuhumiwa lilikuwa wazi na hivyo kuonyesha hali ya kutoamini kuwa watuhumiwa wanaweza kupata dhamana kwa kosa hilo!
Hata hivyo Ofisi ya Mwendesha Mashitaka, DPP haijaweza kulitolea maelezo suala la mahabusu hao kulalamikia mahabusu wenzao kupendelewa katika utoaji wa haki kwa makosa wanayotuhumiwa.


Read more »

Tuesday, 6 May 2014

MARKAZ MISS BAHUL HUDA IMEANZISHWA MNAMO MWAKA 2005



Madrasa hii ilianzishwa mnamo mwaka 2005 ikiwakama madrasa ya nyumbani ikiwa ndani ya jiji la Mwanza katika kito ngoji cha Bugando jeshini  ndaniya wilaya ya nyamagana kwakipindi hicho chote madrasa hii ilkua chin ya mlezi MOHAMED WAZIRIM NA SHEKH WA MADRASA AKIWANI SHEKH AKIDA BIN NASIRI hawa ndio watu wakwanza kabisa kuanzisha madrasa hii kwakipindi kirefu madrasa hii ilika bila ya jina laaina yoyote
Read more »

Saturday, 3 May 2014

Vita vya ndugu kupiganiwa ugenini

   

Timu tatu za Hispania zimefanikiwa kucheza fainali mbili
 tofauti za mashindano yenye hadhi ya juu barani Ulaya mwaka 2014.

Timu hizo mahasimu zimefikia hatua hiyo baada ya Real Madrid
 kuwachabanga waliokuwa mabingwa watetezi wa kombe hilo
 Bayern Munich ya Ujerumani kwa jumla ya mabao 5-0. Real
Madrid ilipata ushindi wa bao 1-0 nyumbani, huku ugenini ikiisambaratisha Bayern magoli 4-0


Nayo Atletico Madrid baada ya kushindwa kuifunga Chelsea katika uwanja wa nyumbani kwa kutoka suluhu ya 0-0, katika mchezo wa marudiano wa nusu fainali katika uwanja wa Stanford Bridge jijini London, Chelsea ilikiona cha moto kwa kuchabangwa magoli 3-1.

Wachezaji wa Atletico Madrid wakishangilia moja ya magoli yao
Hivyo vita vya ndugu hao Real Madrid na Atletico Madrid vitapiganiwa ugenini katika uwanja wa Estádio do Sport Lisboa e Benfica, ujulikanao pia kama Estádio da Luz (uwanja wa mwangaza)mjini Lisbon, Ureno, Jumamosi tarehe 24 Mei 2014.
Kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1967, fainali za kombe la ligi ya mabingwa la UEFA zinafanyika mjini Lisbon.

Baadhi ya wachezaji wa Sevilla walioitoa Valencia
Katika fainali nyingi za kombe la ligi ya Europa, Sevilla ya Hispania inapambana na Benfica ya Ureno mchezo utakaopigwa katika dimba la Turin, nchini Italia Jumatano tarehe 14 Mei 2014.
Sevilla imefuzu kucheza fainali hizo baada ya kuwatoa ndugu zao Valencia katika mchezo wa nusu fainali baada ya matokeo ya 3-3 lakini ikinufaika na goli la ugenini. Katika mchezo wa awali wa nusu fainali, Sevilla iliibuka na ushindi wa 2-0 katika uwanja wake wa nyumbani, lakini ikapata kipigo cha 3-1 ugenini na kufanya matokeo kuwa 3-3.


Read more »

Nigeria kufunga Shule na Ofisi Jumatano


Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan


Rais wa Nigeria Goodluck Jonathana ameagiza shule zote na ofisi za serikali katika mji mkuu wa Abuja nchini humo zifungwe wakati wa siku tatu za Mkutano wa Uchumi wa Dunia World Economic Forum utakaanza nchini humo jumatano ijayo.

Serikali imesema hatua hiyo ni kuarahisisha misafara ya magari. Lakini suala la kuimarisha ulinzi huenda ni mambo yaliyosababisha hatua hiyo Mwandishi wa BBC Will Ross anasema akiwa Abuja.

Ulinzi mkali umehaidiwa kwa wageni wapatao 1000 wakati wa mkutano huo.
Rais Jonathan amesema polisi wapatao 5000 na wanajeshi watafanya doria na kushika hatamu za ulinzi wakati wa mkutano huo utakaoanza wiki ijayo

Waziri Mkuu wa China Li Keqiang na Marais wa Rwanda, Senegal na Kenya ni miongoni mwa viongozi wa juu wa nchi watakaohudhuria.
Mji wa Abuja katika siku arobaini zilizopita ulishambuliwa kwa matukio mawili ya mabomu yaliyoua watu wapatao tisini.

Rais Jonathan amesema polisi wapatao 5000 na wanajeshi watafanya doria na kushika hatamu za ulinzi wakati wa mkutano huo utakaoanza wiki ijayo.





Baadhi ya wanawake wakiandama kutaka serikali kuchukua hatua zaidi kuwaokoa wasichana waliotekwa
Kundi la Boko Haram linadaiwa kuhusika na mashambulizi hayo.
Kundi hilo hilo pia linatuhumiwa kuwateka nyara wasichana zaidi ya 200 katika shule moja kwenye mji wa Borno uliopo Kaskazini Mashariki mwa Nigeria siku arobaini zilizopita.
Jina la kundi hilo lenye tafsiri ya "Kupiga marufuku elimu ya nchi za Maghiribi" kwa lugha ya Kihausa kimekuwa kikiendesha mashambulizi kadhaa kaskazini mwa Nigeria katika siku za hivi karibuni.
   
Baadhi ya wanawake wakiandama kutaka serikali kuchukua hatua zaidi kuwaokoa wasichana waliotekwa
Kundi la Boko Haram linadaiwa kuhusika na mashambulizi hayo.
Kundi hilo hilo pia linatuhumiwa kuwateka nyara wasichana zaidi ya 200 katika shule moja kwenye mji wa Borno uliopo Kaskazini Mashariki mwa Nigeria siku arobaini zilizopita.
Jina la kundi hilo lenye tafsiri ya "Kupiga marufuku elimu ya nchi za Maghiribi" kwa lugha ya Kihausa kimekuwa kikiendesha mashambulizi kadhaa kaskazini mwa Nigeria katika siku za hivi karibuni.



Wanawake walivaa nguo nyekundu kuonyesha kuguswa na wasichana waliotekwa
Inakadiriwa watu wapatao 1500 wameuawa katika mashambulizi yaliyofanywa na kundi hilo pamoja na operesheni ya majeshi ya serikali wakati wa kulisaka kundi hilo.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry ambaye anafanya ziara barani Afrika amesema Marekani itafanya kila liwezekanalo kuisaidia serikali ya Nigeria kuwaokoa na kurudisha nyumbani wasichana mia mbili waliotekwa na kundi la waislamu linalosadikiwa kuwa la Boko Haram siku kumi tisa zilizopita
Read more »

Watatu wauawa kwa bomu Mombasa




Moja kati ya milipuko iliyowahi kutokea Momba
Kenya imekuwa ikikumbwa na matukio ya mashambulio yanayodaiwa kutekelezwa na kundi la kiislamu la Alshabaab la nchini Somalia.
Aidha nchi hiyo imekuwa katika tahadhari tangu mwezi Septemba mwaka jana ambapo wanamgambo wa Alshabaab walivamia kituo cha biashara cha Westgate kilichopo mji mkuu wa Nairobi na kuua watu wapatao 67.
Al Shabaab ni kundi ambalo lina uhusiano na kundi la kigaidi la Al Qaeda ambalo limeapa kulipiza kisasi kufuatia Kenya kutuma majeshi yake nchini Somalia mwaka 2011ambayo yameungana na yale ya Umoja wa Afrika AMISOMsa

Watu watatu wanaripotiwa kuuawa katika mlipuko uliotokea katika mji wa Mombasa nchini Kenya
Kwa mujibu wa taarifa bomu la mkono lilitupwa kwenye basi katika kituo cha mabasi cha Mwembe Tayari
ambalo hupendwa kutembelewa na watalii na kusababisha vifo hivyo na wengine kujeruhiwa

Mlipuko mwingine umetokea katika mtaa wa kifahari wa Nyali.
Kamishna mkuu wa polisi Mombasa, Nelson Marwa, watu 6 wamejeruhiwa na kuwa watu waliotekeleza shambulizi hilo walitoroka kwa Pikipiki.

Read more »

Thursday, 6 February 2014

Taliban wajigamba na Mbwa wa Marekani

Kundi la wapiganaji wa Taleban limesema
 kuwa limemkamata Mbwa kutoka kwa wanajeshi
 wa Marekani Mashariki mwa Afghanistan.

 
Mbwa aliyekamatwa laikuwa anatumiwa 'na kikosi maalum
cha jeshi la Marekani nchini Afghanistan

 Picha waliyoiweka kwenye akaunti yao ya Twitter, inaonyesha Mbwa mdogo wa hudhurungi akiwa na kamba ndogo shingoni.

 Taliban wanasema kuwa Mbwa huyo kwa jina, 'Kanali' alikamatwa usiku wakati wa msako uliofanywa mwezi Disemba.

 Mbwa huyo alikuwa na tochi ndogo, kamera na kifaa cha GPS.


Pia walionyesha silaha walizonasa wakati wa msako huo, ambazo hutumiwa na kikosi maalum cha jeshi la Marekani.
Mwandishi wa BBC anasema kuwa kumekuwa na taarifa za kiongozi wa Taliban katika eneo hilo kuonekana akiwa na Mbwa huyo ambaye sasa ni mfungwa wa kivita.
Read more »

Serikali ya TZ yakana mafao kwa wabunge


 Bunge la Tanzania

 Serikali ya Tanzania imekanusha taarifa za vyombo vya habari zilizodai kuwa wabunge wa nchi hiyo watalipwa kiasi cha zaidi ya dola laki moja za kimarekani watakapomaliza muda wao wa kipindi cha miaka mitano yakiwa malipo ya kiinua mgongo.

 Taarifa ya wizara ya fedha imesema habari hiyo ni ya upotoshaji kwa kuwa Waziri wa fedha ,hakuwahi kuzungumza na mwandishi yeyote kama inavyodaiwa kuwa alithibitisha taarifa hizo.

Read more »

Kenyatta:'Ni aibu lakini hatuna budi'

Maelfu ya watu wanaokabiliwa na uhaba wa chakula nchini
 Kenya wanatarajiwa kupata afueni baada ya Rais Uhuru
 Kenyatta kuzindua rasmi mpango wa kuwapelekea chakula cha msaada.


Rais Kenyatta akizindua msafara wa lori zilizobeba
 chakula cha msaada kwa waathiriwa wa njaa

 Lori kumi na moja ziliondoka Ikulu ya Rais mjini Nairobi zikiwa zimebeba maelfu ya tani za chakuka ikiwemo Mchele, Maharagwe na nafaka zingine ambazo watu wanaokabiliwa na njaa katika sehemu mbali mbali za nchi watafaidika navyo.

Read more »

Habari na U Chambuzi

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com