Monday, 12 May 2014

Kwa Wale Wadada Wa Mjini Wanaopenda Kuvaa Mawigi Katika Vichwa Vyao, Haya Ndiyo Madhara Yake, Tazama Picha Hapa



article-2590565-1C9B48A700000578-713_634x455
Baadhi ya wanawake wengi wa hapa mjini wameanza kutumia style mpya ya kugundisha nywele aka wiving katika vichwa vyao kwa kutumia gundi pasipo kujua mazara yake.
Watafiti na Madaktari kutoka bara ya ulaya wamethibitisha kuwa gundi hizo zinazotumiwa huwa zinakemikali ambayo zinaleta adhari kubwa katika mwili wa mwanadamu hususani kansa. 
 
 
 
Mpaka sasa madaktari bingwa kutoka ulimwenguni kote bado hawajapata uvumbuzi wa dawa ya kutibu kansa zaidi tu ya kutumia njia ya kuchomelea mionzi ili mgonjwa apate ahueni.
 
Read more »

Sunday, 11 May 2014

Marekani yaanza kutumia makombora yenye madin ya yureniam

Read more »

ManCity wanukia ubingwa England

Man City wanaelekea kileleni mwa ubingwa wa ligi ya Uingereza


Ilitarajiwa kwamba Manchester City itapiga hatua, lakini kwa mabao 4 - 0 dhidi ya Aston Villa, ilikuwa kweli mavuno yaliyowarejesha watakapo - kileleni na kuelekea ushindi wa dhahiri wa ligi ya England

Yaya Toure ndiye aliyegonga bao hilo la mwisho, mengine wameyafunga kina Edin Dzeko mabao mawili na Stevan Jovetic bao moja.

Wakiwa na pointi 83 Man City wamewashinda Liverpool kwa pointi mbili na wingi wa mabao
Wanachohitaji sasa ni pointi moja tu watakapokutana na West Ham hapo Jumapili ilhali Liverpool itakutana na Newcastle wakijua vyema kuwa matumaini yao ya kumaliza ukame wa kutwaa kombe hilo wa tangu miaka 24 iliyopita sasa yamefifia labda kutokee miujiza ya Man City wapoteze na wao washinde ndio waibuke na pointi 84.
Katika mechi nyengine Sunderland iliyokuwa mwanzoni inatishiwa kuteremshwa daraja wamenusurika kwa kuichapa West Brom 2-0.
Kwa matokeo hayo imeisukuma Norwich chini ya daraja, ambako imeungana na timu za Fulham na Cardiff katika safari ya kushuka daraja.
Read more »

Cameron:Waliotekwa Nigeria warejeshwe


Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron akiwa na mwandishi wa CNN, Christiane Amanpour katika kampeni ya kutaka wasichana waliotekwa Nigeria waachiliwe haraka.

Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron ameahidi Uingereza "kufanya kile itakachoweza" kusaidia kuwapata wasichana wa shule zaidi ya 200 waliotekwa na magaidi wa Boko Haram.
Bwana Cameron amesema hayo wakati alipopokea karatasi ya iliyosainiwa kauli mbiu"#Bring Back Our Girls" yaani warejeshe wasichana wetu, wakati wa kipindi cha BBC cha Andrew Marr.

Bwana Cameron ni kiongozi wa hivi karibuni wa juu kuunga mkono kampeni ya vyombo vya habari vya mitandao ya kijamii baada ya mke wa rais wa Marekani Michelle Obama alipopigwa picha kiwa na karatasi yenye maandishi kama hayo.

Wapiganaji wa Kiislam wa kikundi cha Boko Haram wamedai kuhusika na utekaji wa wasichana hao.
Wakati wa programu hiyo ya BBC, mgeni mwaalikwa Christiane Amanpour, mwandishi wa habari mkuu wa kimataifa wa CNN, alimkabidhi bwana Cameron karatasi lenye maandishi ya "#Bring Back Our Girls" na kumwuliza kama angependa kujiunga na kampeni hiyo.

Baadaye Bwana Cameron alituma ujumbe kwa njia ya tweeter: "Ninafuraha kuunga mkono kampeni ya #BringBackOurGirls."
Waziri mkuu huyo wa Uingereza alikiambia kipindi cha BBC One programme: "nilimpigia simu rais wa Nigeria kusaidia chochote ambacho kingwezesha kupatikana kwa wasichana waliotekwa na tumekubaliana kutuma timu ya wataalam wakiwemo wa kukabiliana na vitendo vya ugaidi na ujasusi ili kufanyakazi kwa pamoja na timu kubwa ya wataalam wa Marekani wanaokwenda huko.

"Tuko tayari kufanya lolote zaidi ambalo Wanigeria watataka tufanye."
Amesema huenda Nigeria isiombe msaada wa majeshi ya Uingereza lakini amesema: "Nimemwaambia Rais Jonathan, pale tutakapoweza kusaidia, tafadhali aseme, na tutaona tukachoweza kusaidia."
Mke wa Rais wa Marekani, Michelle Obama amekuwa akipiga kampeni ya kuachiliwa kwa wasichana waliotekwa.
Wapiganaji wa Boko Haram
Bwana Cameron pia amezungumzia umuhimu wa kukabiliana na misimamo mikali ya itikadi za kidini duniani kote.
"Hili si tatizo tu la Nigeria," amesema. "Kwa kweli tunaona misimamo hii mikali ya Uislam- tunaona matatizo Pakistan, tunaona matatizo katika maeneo mengine ya Afrika, matatizo Mashariki ya Kati.

"Pia, hebu tu wakweli, hapa Uingereza bado kuna vikundi vyenye kuunga mkono misimamo mikali ya kidini, ambayo tunatakiwa kukabiliana nayo, iwe mashuleni, vyuoni au vyuo vikuu na kwingineko.."
Anaelewa kuwa si kazi rahisi kuwatafuta wasichana, ambao walitekwa kutoka shuleni kwao Chibok tarehe 14 Mei 2014 katika jombo la Borno.
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis pia naye ametuma ujumbe wa tweeter akiunga mkono kampeni ya kurejeshwa wasichana hao akiandika: "tuungane katika maombi ili kuachiliwa haraka kwa wanafunzi hao wa kike waliotekwa nchini. #BringBackOurGirls."



Read more »

Mapigano yazuka upya Sudan Kusini

Salva KIir (kushoto) na Riek Machar wakipeana mkataba waliotia saini Addis Ababa
Serikali na wapiganaji wa Sudan Kusini wamelaumiana kwa kuvunja makubaliano ya kusitisha mapigano - masaa tu baada ya makubaliano kufikiwa

Msemaji wa jeshi la serikali, Kanali Philip Aguer, alisema wapiganaji wameshambulia maeneo ya serikali katika mji wa Bentiu leo alfajiri.
Wapiganaji wamewashutumu wanajeshi wa serikali kuwa waliwashambulia katika sehemu kadha katika majimbo ya Upper Nile na Unity.
Makubaliano ya kusitisha mapigano yalitiwa saini Ijumaa, na yalikusudiwa kumaliza vita vya miezi mitano ambavyo vimeuwa maelfu ya watu na kulazimisha zaidi ya milioni moja kuhama makwao.

Taarifa zinazohusiana

Read more »

Mradi wa reli mpya watiwa saini Nairobi

Waziri mkuu wa Uchina Li Keqiang

Waziri Mkuu wa Uchina, Li Keqiang, na viongozi wa Afrika Mashariki wametia saini rasmi makubaliano ya kujenga njia mpya ya reli itayounganisha mji wa Kenya wenye bandari, Mombasa, hadi Nairobi, Rwanda na Sudan Kusini.

Waziri Mkuu wa Uchina yuko mjini Nairobi akiwa katika ziara ya Afrika.
Njia hiyo ya reli ya upana unaotumika kawaida duniani itagharimu mabilioni ya dola, na itachukua nafasi ya njia ya reli ya sasa ambayo ni nyembamba na ilijengwa zama za ukoloni wa Uingereza.
Sehemu ya kwanza ya reli itajengwa na kampuni za Uchina - jambo lilozusha malalamiko kwamba kampuni nyengine hazikuruhusiwa kushiriki katika kuomba kandarasi.
Read more »

Saturday, 10 May 2014

Tazama Picha 10 Za Mahabusu Walioamua Kuvua Ngua Na Kubaki Watupu Kama Walivyozaliwa Huko Jijini Arusha..!!

Inspector Henry akiwasihi mahabusu hao wawili wanaotuhumiwa kwa kesi za mauaji, kuachia mlingoti wa Bendera ya Taifa na kurudi kwenye chumba cha mahakama kwaajiri ya taratibu za kesi.

Matukio ya ajabu yanayofanywa na mahabusu wanaoshinikiza kesi zao kusikilizwa haraka ikiwa ni mbinu wanazoamini zitasaidia katika kile wanachoeleza kuwa ni kudai haki zao yanaendelea kuonekana ambapo jana mahabusu jijini Mwanza walifanya tukio la aina yake.
 
Mahabusu wawili kati ya sita wanaoshikiliwa kwa tuhuma za mauaji jana walijaribu kutoroka kutoka kwenye mstari wa utaratibu wa kuingia mahakamani na kisha kung’ang’ania mlingoti wa bendera ya Taifa huku mmoja wao akivua nguo zote na kubaki mtupu.
 
Tukio hilo lilitokea majira ya saa nne asubuhi katika Mahakama ya Hakimu Mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Nyamagana, jijini Mwanza.
 
Thobias Warioba, mmoja kati ya mahabusu hao ndiye aliyevua nguo zote na kubaki mtupu na kisha kupiga kelele akiwa ameshikilia mlingoti akieleza kilio chake.
 
“Haiwezekani tangu mwaka 2011 tulipokamatwa hadi sasa kesi zetu hazijasikilizwa. Wengine tumebambikiwa kesi. 

"Tunaomba haki zetu, polisi wanatuonea, vyombo vya habari tunaomba mtusaidie tumekaa muda mrefu bila kusikilizwa na hatujui hatma yetu tangu mwaka 2011tulipokamatwa.

"Tumechoka kukaa mahabusu, tunaomba kesi zetu zisikilizwe.” Alisema Thobias Warioba.
 
Inspector wa polisi alijitambulisha kwa jina la Henry aliwataka watuhumiwa hao waondoke katika mlingoti na kuvaa nguo ili waingie mahakamani kwani kitendo walichokuwa wakikkifanya ni kosa la jinai..
 
“Pamoja na maamuzi yenu haya, lakini mtambue mnavunja sheria na hili ni kosa jingine la jinai, hivyo ni vyema mkaondoka kwenye mlingoti huu na kuingia mahakamani. Malalamiko yenu tumeyasikia na yatashughulikiwa.” Alisema Inspecta Henry.
 
 
Askari polisi wakiwalinda mahabusu wawili kati ya sita wanaotuhumiwa kwa kesi za mauaji
 
 
Inspector Henry (shati la bahari) akiwa na Inspector Veda (mwenye koti) wakisikiliza hoja za Thobiasi Warioba (35), aliyeamua kuvua nguo zote na kubaki mtupu akiwa ameng’ang’ania mlingoti wa Bendera ya Taifa
 Ushawishi ukiendelea
 Mahabusu Thobiasi Warioba (aliye mtupu) pamoja na mwenzake Hamis Ramadhani katu katu waking’ang’ania mlingoti wa bendera ya Taifa huku wakishinikiza kuzungumza na waandishi wa Habari.
 Baada ya kuzungumza na waandishi wa habari mahabusu hao walikubali kurejea chumba cha Mahakama.
 Mashuhuda
 
Nae mmoja wa maafisa wa mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza ambaye hakutaka jina lake litajwe, alieleza kuwa ushahidi wa kesi za watuhumiwa hao bado haujakamilika na kwamba kesi zao haziwezi kusikilizwa na mahakama ya Wilaya kwani haina uwezo, na badala yake zitaendelea kutajwa tu kisha zitahamishiwa Mahakama Kuu.
 
 
 
 

Read more »

Mfahamu Tajiri Namba Moja Hapa Tanzania Mwenye Mabilioni Na Mabilioni Ya Pesa ?


Chama Cha Mapinduzi (CCM) party stalwart Rostam Aziz has earned USD 240 million (about Tsh. 384,000,000,000/-) from selling part of his stake in Tanzania’s largest mobile phone company, Vodacom Tanzania.
Rostam Aziz has made the fortune by selling 17.2% of his 35% shares in Vodacom Tanzania, the business magazine Forbes has reported.

Rostam owns part of Vodacom through the company Cavalry Holdings, a Jersey island-registered private investment company wholly controlled by the Tanzanian politician.In an article carrying the headline “Tanzania’s Richest Man Concludes Sale Of Vodacom Stake”, Forbes has published the following report:Vodacom Group Ltd, the African subsidiary of British telecoms giant Vodafone announced on Tuesday that it has finally concluded its acquisition of an additional indirect 17.2% interest in Vodacom Tanzania previously owned by Tanzania’s richest man, Rostam Azizi.

In a press release statement, the company said it had fulfilled all requirements as mandated by the Tanzanian regulatory authorities and that the transaction was now unconditional.“As all the conditions precedent to the transaction have been fulfilled, the transaction is now unconditional and closing is expected to take place today, 29 April 2014,” the company said.

Last November, Vodacom announced it would spend up to R2.5 billion ($240 million) to acquire a 17.2% stake in Vodacom Tanzania from Cavalry Holdings, a Jersey island-registered private investment company wholly controlled by Rostam Azizi. Cavalry previously held a 35% in Vodacom Tanzania.

With this acquisition, Cavalry’s holding the company is now reduced to 17.8%, while Vodacom Group, a Johannesburg Stock Exchange-listed entity that previously owned a 65% stake in the company will now own 82.2%. Vodacom Tanzania, which has more than 10 million active subscribers, is the country’s largest mobile phone company, and Vodacom Group’s second most successful operation in Africa, after its South African unit that boasts more than 23 million subscribers.

Azizi, 49, is Tanzania’s first billionaire with a fortune estimated at $1 billion, derived from stakes in contract mining firm Caspian Mining, a Port in Dar es Salaam, extensive real estate in Tanzania and the Middle East and, of course, cash coming from the sale of his stake in Vodacom Tanzania


Read more »

Thursday, 8 May 2014

ANGALIA MWILI WA FIRAUN-LANA TULLAH


                           FIRAUN LANATULLAH  
Read more »

Je Marekani imechelewa kusaidia Nigeria?








Michele Obama emejiunga na kampeni hii kutaka kuachiliwa kwa wasichana wa Nigeria

Wiki tatu tangu wasichana zaidi ya miambili kutekwa nyara na Boko Haram nchini Nigeria, Jana ndio Marekani ilitangaza kutuma kikosi maalum kusaidia Nigeria kuwatafuta wasichana hao

Je kimya hiki kilichukua muda mrefu kwa nini, jee kujihusisha kwa Marekani wakati huu kutasaidia hali?

Matukio machache yametendeka huku dunia nzima ikichukua muda kujibu mfano ikiwa hii taarifa ya kutekwa kwa wasichana wa Nigeria kutoka katika shule yao ya mabweni Kaskazini mwa Nigeria.

Maandamano yamefanyika mjini New York, Los Angeles na London,wakati ujumbe mwingi kupitia kwenye mitandao ya kijamii ikitolewa sio tu kwa Boko Haram bali pia kwa serikali ya Nigeria kwa kuonekana kama isioguswa na tukio hilo.
Mnamo siku ya Jumatano, mke wa Rais wa Marekani Michelle Obama alituma ujumbe kwa Twitter uliosema 'BringBackOurGirls' yaani ''#Turudishieni wasichana wetu'' kuongeza sauti yake kwa kampeini ambayo imewaka moto dunia nzima.


Ni wiki tatu tangu kutekwa nyara kwa wasichana wa Nigeria. Boko Haram imesema
 itawauza wasichana hao
Hii ni kamepin iliyoanza nchini Nigeria kuwataka Boko Haram kuwaaachilia wasichana hao.
Mchango wake kwa kampeini hii umekuja siku moja baada ya Marekani kutangaza kupeleka kikosi kusaidia Nigeria. Kikosi hicho kitasaidia Nigeria kwa upande wa
uchunguzi, kuzungumza na wapiganajji kuwashawishi kuwaachilia wasichana na kuwasaidia waathiriwa.
Alipouliozwa kwa nini ilichukua mda mrefu, waziri wa mambo ya kigeni John kerry alijibu kuwa Marekani ilikuwa imejitolea kusaidia lakini serikali ya Nigeria ikawa haiko tayari kwa hilo.
"tumekuwa tukishauriana tangu tukio hilo kuripotiwa, lakini inaonekana serikali ya Nigeria ilikuwa na mikakati yake, '' alisema Kerry.
Lakini jibu hilo halijawakomesha watu kuuliza, kwa nini nchi za magharibi zimejikokota katika kusaidia Nigeria kama vile, Ufaransa, Uingereza na Marekani? Hata hivyo licha ya malalamiko haya msemaji wa serikali ya Uingereza amekanusha madai kuwa nchi hizo zimechelewa kusaidia Nigeria.
Baadhi ya wachanganuzi wamefananisha kuchelewa kwa mataifa hayo kusaidia Nigeria kinyume na ilivyokuwa wakati ndege ya Malaysia MH370 ilipopotea huku mataifa mengi tu yakijitolea kusaidia Malaysia.
Wakati mwingine bara la Afrika linaweza kuwa giza kuu kwa mataifa ya Magharibi , lakini sio kwa wakati huu ambapo msaada mkubwa unahitajika.
Read more »

INNA LLAHI WA INAILAIKA RAJIUN

683 wahukumiwa kifo nchini Misri.

Jali alipokuwa anatoa hukumu, jamaa na familia za watuhumiwa walikuwa nje
 ya mahakama tayari kupokea hukumu dhidi ya wapendwa wao


Jali alipokuwa anatoa hukumu, jamaa na familia za watuhumiwa walikuwa nje ya mahakama tayari kupokea hukumu dhidi ya wapendwa wao

 


Mahakama nchini Misri hii leo imetoa hukumu ya kifo kwa watu wanaoshukiwa kuwa wanachama wa vuguvugu la Muslim Brotherhood.


Polisi walilazimika kuweza kizuizi hiki ili kuzuia watu kuingia upande wa mahakama. Serikali tangu hapo imekuwa ikiwasaka watu wanaoshukiwa kuwa wanachama wa Muslim Botherhood ambao rais wao aliondolewa mamlakani na jeshi
Read more »

Habari na U Chambuzi

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com