Monday 19 May 2014

Wanawake waomba mapadre waoe

Posted by mkachu  |  Tagged as:

Kundi moja la wanawake walio na hisia za kimapenzi na mapadre wa kikatoliki wamemuandikia barua kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis ya kumtaka kubadilisha sheria za kanisa hilo zinazowazuia viongozi hao wa dini kuoa.    




Papa Francis kiongozi wa kanisa katoliki

Wanawake hao 26 kutoka Italy na maeneo mengine wanasema kwamba wamekuwa wakishiriki ama wanataka kushiriki katika uhusiano wa kimapenzi na mapadre na kwamba wametoa ombi hilo kwa niaba ya wanawake wengine ambao wako katika hali kama hiyo

Barua hiyo inazungumzia kuhusu uchungu wa kushindwa kuishi maisha yao kikamilifu mbali na kutaka kukutana na papa Francis.
Papa Francis amekuwa akiunga mkono utamaduni wa ujane,lakini mwaka 2010 aliandika akisema kuwa huenda msimamo wake ukabadilika.
Papa francis amekuwa akimtembelea mjane wa aliyekuwa kasisi Jeronimo Podesta ambaye alijiuzulu katika utumishi wake na kuoa, zaidi ya miaka 40 iliopita.

Habari na U Chambuzi

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com