Tuesday 20 May 2014

Tanzania yaibamiza Zimbabwe 1 - 0

Posted by mkachu  |  Tagged as:

 
 Timu ya Tanzania Taifa Stars

Michuano ya soka kuwania Tiketi ya kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa barani Afrika hapo mwakani nchini Morocco imeanza mwishoni mwa wiki hii kwa mechi kadhaa barani Afrika ambapo katika mechi iliyochezwa jijini Dar es Salaam Tanzania, Taifa Stars imeilaza Zimbabwe bao 1-0.

Bao hilo pekee na la ushindi la Taifa Stars limetiwa kimiani mapema na Mshambuliaji John Bocco kufutaia krosi ya Thomas Ulimwengu kutoka wingi ya kulia ikiwa ni dakika ya 14 ya mchezo.

 Kwa upande wake nahodha wa taifa Stars anasema ushindi huo japo ni mwembamba lakini si jambo dogo kwa sababu wanaweza kupata bao la ugenini mapema na kasha kuweza kupangilia namna na kulinda ushindi huo.


Naye Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayesukuma ngozi kwenye klabuya TP Mazembe ya Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo anasema kwa kiasi Fulani kucheza mechi mbili ndani ya saa 48,baada ya Ijumaa kucheza dhidi ya Al Hilal ya Sudan kwa kiasi Fulani kulimchosha kimchezo na hivyo kushindwa kuitumikia vema Tanzania kuweza kuipatia ushindi.
Kufuatia ushindi huo Mwembamba Kocha wa Tiofa Stars mholanzi Marti Noij anasema
Si kwamba sisi ni Tanzania wazuri sana kuliko Zimbabwe au kwamba wao ni wazuriu sana kulikosisi kiuwezo,lakini mechi ijayo itakuwa ngumu na naamini timu itakayotumia nafasi itakazopata vema ndiyo itaibuka na ushindi,mechi itakuwa ngumu kwa sasabu huu ni mtoano.
Naye Kocha wa Zimbabwe Ian Gorowa anasema, kufuatia majeruhi wengikatika kikosi chake waliwamua waliamukuwapa nafasi vijana chipukizi ambao walionyesha uwezo mkubwa na akakiri kuwa Tanzania ni timu nzuri na nawapongeza lakini mechi ijayo mjini Harare ndiyo itaamua nanio anasonga mbele.
Kwa matokeo hayo Tanzania itahitaji sare ya namna yoyote ili kusonga mbele katika raundi ya pili kuelekea kusaka tiketi ya Moroco hapo mwakani,baada kuzikosa Fainali za Matifa Afrika kwa zaidi ya miaka 34,
Naye Mdau mwingine wa soka nchini ambaye pia ni Mbunge wa chama cha upinzanii Chadema Zitto Kabwe pamoja na ushindi huo mwembamba anasema Taifa Stars inafaa kuungwa mkono kwa mechi ya marudiano mjini Harare.

Habari na U Chambuzi

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com