Wednesday, 29 January 2014

Taarifa mpya kuhusu shambulizi Nigeria

Taarifa mpya zimeibuka kuhusu shambulizi
 lililofanywa dhidi ya kanisa moja katika eneo
la kaskazini mashariki mwa Nigeria siku ya Jumapili.

Kundi la Boko Haram limelaumiwa kufanya mashambulizi
 mengi Kaskazini mwa nchi

Askofu wa kanisa hilo Yola, Mamza Dami Stephen, ameiambia BBC kuwa wapiganaji walilifunga kanisa hilo, katika kijiji cha Waga Chakawa, baada ya misa na kuwapiga risasi wale wote waliojaribu kutoroka kwa kupita kwenye madirisha.
Inaarifiwa takriban watu 30 waliuawa kwa njia hiyo.

Siku hiyo hiyo washambuliaji walivamia kijiji cha Kawuri na kuwaua watu 52. Kundi la Boko Haram limelaumiwa kwa kufanya mashambulizi hayo.
Amesema kuwa baadhi yao walikatwa koo zao. Takriban watu thelathini walifariki kufuatia shambulizi hilo ambalo inasemekana limesababishwa na kundi la wapiganaji wa kiislamu la Boko Haram.
Shambulizi lingine liliwaacha watu hamsini wakiwa wamefariki katika jimbo la Borno.
Wapiganaji wa Boko Haram wanataka kutawala kutumia sheria za kiisilamu katika nchi ambayo imegagawanyika kati ya wasilamu na wakristo.
Kundi hilo limewaua maelfu ya watu katika kipindi cha miaka minne iliyopita, huku kundi hilo likisemekana kuwa tisho kubwa sana kwa taifa hilo lenye utajiri mkubwa wa mafuta.
Majimbo ya Borno na Adamawa pamoja na jimbo la Yobe yako chini ya sheria ya hali ya hatari tangu mwezi Mei mwaka jana huku jeshi likijaribu kupambana na wapiganaji hao wa kiisilamu.
Read more »

Jaribio la kumuua waziri Libya latibuka

Kumekuwa na jaribio lililotibuka la kumuua kaimu
  waziri wa ndani nchini Libya Al-Sidik Abdel-Karim.

Shirika la kitaifa la habari LANA na lile la AFP
 yamethibitisha tukio. Inaarifiwa kwamba gari                    
alimokuwa Abdel Karim lilipigwa risasi alipokuwa
akielekea katika mkutano katika makao makuu ya bunge.

Libya imekuwa ikikumbwa na msukosuko wa kisiasa tangu Muamar Gadaffi kuuawa

Abdel-Karim anatarajiwa kuhutubia waandishi habari hivi punde.
Abdel-Karim anatarajiwa kuhutubia waandishi habari hivi punde.
Abdel Karim aliteuliwa na waziri mkuu nchini Libya kuwa kaimu waziri wa ndani baada ya waziri Mohamed Sheikh kujiuzulu mnamo Agosti mwaka jana.
Seddik Abdelkarim, alikuwa katika gari lake aliposhambuliwa na watu wasiojulikana waliomfyatulia risasi. Inaarifiwa hakuna aliyeuawa kwenye shambulizi hilo.
Libya imekuwa ikikabiliwa na hali ngumu ya kisiasa tangu waasi kuipindua serikali na kumuua aliyekuwa Rais Muamer Kadhafi mwaka 2011.
Waziri huyo alikuwa njiani kuelekea bungeni wakati gari lake liliposhambuliwa.
Shambulizi lenyewe limetokea chini ya wiki tatu baada ya mauaji ya naibu waziri wa viwanda Hassan al-Droui, aliyeuawa mjini Sirte
Read more »

Viiongozi wa waasi kushitakiwa S.Kusini


 
 Maelfu waliachwa bila makao kutokana na vita Sudan Kusini

Serikali ya Sudan Kusini imesema kuwa itawahukumu wahusika wakuu wa njama ya mapinduzi dhidi ya serikali ya Rais Salva Kiir.

Serikali ya Kiir, imesema kuwa njama hiyo ndiyo iliyosababisha mapigano kati ya serikali na waasi waliokuwa wanaongozwa na Riek Machar.
Baadhi wanahofia kuwa hatua hii huenda ikasababisha uhasama zaidi na kutishia mkataba wa amani kati ya waasi na serikali.
Pande zote mbili kwenye mgogoro wa Sudan Kusini zilitia saini mkataba wa kusitisha vita Ijumaa iliyopita, lakini vita vimepungua tu bali havijasitishwa.
Duru zinasema makabiliano yangali yanaendelea huku zaidi la watu 800,000 wakilazimika kutoroka makwao.

Read more »

Monday, 27 January 2014

Uhuru una maana gani?








Thailand ndio nchi ya tatu duniani inayoongoza kwa kusafirisha nje mazao ya baharini na inasambaza kwenye maduka makubwa nchini Marekani na katika nchi za Umoja wa Ulaya, EU.

Muziki wa kijeshi unasikika kwa sauti kubwa.

 Mbele yetu wako maafisa wa polisi 100 wakiwa wamejipanga mstari. Jenerali Chatchawal Suksomjit, Naibu Mkuu wa Polisi, anapita karibu na askari waliojipanga akisalimiana nao na kupiga saluti.
Akiwa amevalia miwani yake myeusi na sare za kijivu anaashiria jambo muhimu. Anatuamuru kuelekea kwenye boti za polisi zinazosubiri kwenye mwambao wa Malacca karibu na mpaka na Malaysia.
Jenerali huyo ni mkuu mpya wa kamati iliyoundwa kushughulikia tatizo la usafirishaji wa wanaume kwenda kwenye biashara ya uvuvi, sekta anayoielezea kuwa ni ‘hatari, ngumu na isiyofaa’.

 Tatizo kubwa tunaloliona ni kwamba, endapo watu hawatafanya kazi wanakuwa hawana maana ndani ya boti, wanaweza kuuawa na kutoswa baharini,” anasema. Haitokei katika kila boti lakini inatokea sana hivyo kuzua maswali mazito kuhusu kukosekana kwa sheria katika sekta hii.”

 Pia kuna tatizo la uhaba wa ajira. Kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Kazi, sekya uvuvi nchini Thailanda ina upungufu wa ajira 50,000. Nahodha mmoja katika bandari ya Chonburi anasema wanataabika.

Kimsingi, mfanyakazi haramu kutoka Cambodia au Burma hukutana na dalali na hupatiwa ajira ya kiwandani. Anaikubali na hujikuta akitambulishwa kutoka kwa dalali mmoja hadi mwingine, na kasha hupelekwa bandarini na kupandishwa ndani ya boti. Na baada ye huambiwa anadaiwa pesa nyingi.
Ni mtego wa hatari. Endapo atatoroka, kama mhamiaji asiyeandikishwa polisi watamkamata na kumrejesha kwao. Mwanaume mmoja kutoka Cambodia niliyezungumza naye alitumikishwa kwenye boti kwa miaka mitatu bila kulipwa ujira wake, akadanganya kuwa pesa yote kalipa madeni. Hakuwahi kuambia kiasi anachodaiwa.
Jenerali na wasaidizi wake hawawezi kuzungumza moja kwa moja na baharia wa Burma kwa sababu hawajaleta mkalimani hivyo inawawia vigumu kutambua kama watu hao wamesafirishwa kiharamu.
“Si ingekuwa kazi rahisi kama mngekuwa na mkalimani?” Nauliza. Anajibu kwa kawaida wanategemea mtu anayekuwepo ndani ya boti ambaye anaweze kuzungumza lugha ya Burma, kama nahodha pengine. Hata hivyo, mara nyingi ni nahodha ndiye anayetuhumiwa kwa unyanyasaji na utesaji.
‘Ni kwa vipi mnaweza kutambua kwamba, hapa hakuna watu waliosafirishwa kiharamu ama kulazimishwa kufanya kazi?’ Nauliza tena.
‘Kwa jinsi tulivyoshuhudia, hakuna chumba wala mahabusu ya kuwahifadhi watu wanaokamatwa,’ anasema. ‘Hatukuona alama zozote za majeraha kwenye miili yao ama nyuso zao. Kwa kuangalia nyuso zao na macho hawaonekani kama walilazimishwa kufanya kazi.’
Wakati mamlaka inapowaokoa watu waliosafirishwa kiharamu, mara nyingi huwahifadhi katika kituo cha serikali nje ya mji mkuu wa Bangkok.
Ken ni mmoja wa watu hao. Anaeleza kwamba, aliahidiwa kazi nzuri ya kiwandani lakini akalazimishwa kupanda boti ndogo baharini ambako alifanya kazi ya uvuvi kwa saa 20 kwa siku, siku saba za wiki. Dalali anasema kwamba, Ken alikuwa akidaiwa fedha nyingi baada ya kupatiwa ajira na kupelekwa bandarini. Miezi ikapita na Ken, kama walivyo wengine wengi hakulipwa pesa yake.

Read more »

Kiongozi wa Al Shabaab ashambuliwa

eshi la Marekani limefanya shambulizi la makombora dhidi ya mtu anayeshukiwa kuwa mmoja wa viongozi wa al-Shabaab nchini Somalia.  

Jeshi la Marekani limefanya shambulizi la makombora dhidi ya mtu anayeshukiwa kuwa mmoja wa viongozi wa kundi la wanamgambo la al-Shabaab nchini Somalia.

Maafisa katika idara ya ulinzi wanasema kuwa wanajaribu kubaini ikiwa shambulizi hilo lilimuua mlengwa ambaye jina lake halijatajwa

Read more »

Friday, 24 January 2014

Syria yatishia kujiondoa Geneva

Waziri wa mambo ya nje wa Syria, Walid Muallem, ametoa tisho la kujiondoa kwenye mazungumzo ikiwa hakuna hatua zitakazokuwa zimefikiwa Jumamosi

 Mamilioni ya watu wameachwa bila makao kutokana na vita nchini Syria
 Waakilishi wa serikali ya Syria katika mazungumzo ya amani kati ya wanaharakati na serikali, wametishia kuondoka kwenye mazungumzo hayo ya amani ikiwa mazungumzo muhimu hayatakuwa yameanza ifikapo Jumamosi.
Read more »

5 wauawa kwenye mashambulizi Cairo

Milipuko mitatu imetikisa mji mkuu wa Misri, Cairo
 na kuwaua watu 5 huku zaidi ya tisini wakijeruhiwa.       
Mlipuko umetokea wakati wa kuadhimisha siku ya kuondolewa mamlakani kwa Hosni Mubarak

Milipuko mitatu imetikisa mji mkuu wa Misri, Cairo na kuwaua watu 5 huku zaidi ya tisini wakijeruhiwa.
Mlipuko mkubwa wa kwanza ulitokana na bomu lililokuwa limetegwa ndani ya gari, lililokuwa limeegeshwa nje ya kituo cha polisi.
Kundi lenye uhusiano na Al-Qaeda, Ansar Beit al-Maqdis, limekiri kutekeleza mashambulizi hayo


Milipuko mingine miwili ilitokea nje ya kituo kimoja cha magari na kusababisha majeruhi.
Duru zinasema kuwa watu wawili waliojihami kwa bunduki waliwashambulia walinzi katika jengo hilo la polisi.
Kituo cha televisheni cha Serikali kimesema kuwa milio ya risasi ilisikika mara tu baada ya milipuko hiyo.
Moshi ulionekana ukifuka juu ya majengo katikati mwa mji na picha za televisheni zilionyesha uharibifu mkubwa wa majengo hayo.
Zaidi ya ambulansi 30 zimepelekwa eneo hilo kushughulikia waathiriwa. Mlipuko huo umetokea katika siku ya kuadhimisha miaka mitatu tangu kupinduliwa kwa Hosni Mubarak.
Read more »

Thursday, 23 January 2014

INAA LIKKAHI WA INNA ILAHI RAAJIUON

Read more »

Habari na U Chambuzi

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com