Thursday, 6 February 2014

Kenyatta:'Ni aibu lakini hatuna budi'

Posted by mkachu  |  Tagged as:

Maelfu ya watu wanaokabiliwa na uhaba wa chakula nchini
 Kenya wanatarajiwa kupata afueni baada ya Rais Uhuru
 Kenyatta kuzindua rasmi mpango wa kuwapelekea chakula cha msaada.


Rais Kenyatta akizindua msafara wa lori zilizobeba
 chakula cha msaada kwa waathiriwa wa njaa

 Lori kumi na moja ziliondoka Ikulu ya Rais mjini Nairobi zikiwa zimebeba maelfu ya tani za chakuka ikiwemo Mchele, Maharagwe na nafaka zingine ambazo watu wanaokabiliwa na njaa katika sehemu mbali mbali za nchi watafaidika navyo.



Hatua ya Rais Kenyatta inakuja wiki moja baada ya halmashauri ya kitaifa ya kupambana na ukame kuonya serikali kuhusu tisho la uhaba wa chakula ikisema kuwa majimbo 11 yenye zaidi ya watu milioni moja yanakabiliwa na tisho hilo la uhaba wa chakula.
Kenyatta alikiri kuwa ni aibu kubwa kuwa nchi hiyo inatoa msaada wa chakula kwa raia wake ishara kuwa hapakuwa na mipango yoyote kuweza kuzuia hali hii.
Hata hivyo amesema kuwa serikali haina budi ila kufanya hivyo.
Ameelezea kuhusu mipango tofauti ya serikali inayonuia kukabiliana na tatizo la uhaba wa chakula ikiwemo kuanzisha miradi ya kukuza chakula, miradi ya unyunyiziaji mimea maji na miradi mingine kuhakikisha kuwa Kenya ina uwezo wa kutosha kujilisha.
Maeneo yanayokabiliwa na tisho la njaa ni pamoja na Samburu, Turkana, Garissa, Mandera, Wajir, Isiolo, Marsabit, Pokot, Baringo, Tana River jimbo na maeneo ya Lamu .
Waziri wa ugatuzi Ann Waiguru amesema kuwa chakula kingine cha msaada kinatarajiwa kupelekewa waathiriwa katika wiki chache zijazo.
Rais Kenyatta amesisitiza kuwa chakula kitaendelea kupelekwa hadi pale hali itakapokuwa sawa akisema kuwa mamilioni ya dola imetengwa kuhakikisha kuwa watu wanaokabiliwa na njaa

Habari na U Chambuzi

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com