Bunge la Tanzania
Serikali ya Tanzania imekanusha taarifa za vyombo vya habari zilizodai
kuwa wabunge wa nchi hiyo watalipwa kiasi cha zaidi ya dola laki moja za
kimarekani watakapomaliza muda wao wa kipindi cha miaka mitano yakiwa
malipo ya kiinua mgongo.
Taarifa ya wizara ya fedha imesema habari hiyo ni ya upotoshaji kwa kuwa
Waziri wa fedha ,hakuwahi kuzungumza na mwandishi yeyote kama
inavyodaiwa kuwa alithibitisha taarifa hizo.
Baada ya kuzuka kwa taarifa hizo baadhi ya wabunge waliozungumza na
vyombo vya habari walikiri kuwepo kwa mipango hiyo huku wengine
wakikanusha kuwa hawajawahi kupitisha mapendekezo kama hayo bungeni.
Naye naibu spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai ameiambia BBC kuwa
habari hizi si za kweli '' nipende kusema kuwa jambo hilo kwa kweli si
la kweli.Si la kweli kwa sehemu mbili,kwanza kwa utaratibu wa utawala
wetu bora Tanzania, hakuna mtu mwenye mamlaka ya kujiongezea yeye
mwenyewe kipato chake katika utumishi wa uma.kila ambaye ana mshahara au
marupurupu ya aina fulani lazima yaidhinishwe na mamlaka au chombo
kingine, ndio utaratibu wa utawala wetu.Kwa hiyo na sisi Bunge hatuna
mamlaka ya kujipangia posho ya aina yoyoyte au mshahara wa aina yoyote
kwa wabunge au viongozi wa Bunge''.
Pia naibu spika Ndugai amesema madai ya baadhi
ya Wabunge kuwa kulikuwa na mpango huo si ya kweli na hayajawahi
kujadiliwa katika Bunge hilo.
Taarifa hizo zilisababisha malalamiko kutoka kwa
wananchi kuhusu hatua ya serikali kuwapatia wabunge kiasi hicho kikubwa
cha fedha huku ikidai kuwa haina fedha za kutekeleza miradi kwa ajili
ya huduma nyingine za umma.
Thursday, 6 February 2014
Browse: Home
» Serikali ya TZ yakana mafao kwa wabunge
Serikali ya TZ yakana mafao kwa wabunge
Posted by mkachu |  Tagged as:
Habari na U Chambuzi
HALI YA HEWA
TANGAZANASI
MTANDAO WA KIJAMII
ZILIZO SOMWA ZAIDI
-
Chama Cha Mapinduzi (CCM) party stalwart Rostam Aziz has earned USD 240 million (about Tsh. 384,000,000,000/-) from selling part of his st...
-
eshi la Marekani limefanya shambulizi la makombora dhidi ya mtu anayeshukiwa kuwa mmoja wa viongozi wa al-Shabaab nchini Somalia. ...
-
Wanaume wengi wanapofikia hatua ya kuoa si kwamba wanakurupuka tu na kuoa mwanamke yeyote mwenye sura nzuri, bali huchukua muda wao mw...
-
Baadhi ya wanawake wengi wa hapa mjini wameanza kutumia style mpya ya kugundisha nywele aka wiving katika vichwa vyao kwa kutumia gu...
-
683 wahukumiwa kifo nchini Misri. ...
-
Maelfu ya watu wanaokabiliwa na uhaba wa chakula nchini Kenya wanatarajiwa kupata afueni baada ya Rais Uhuru Kenyatta kuzindua rasmi m...
-
Kumekuwa na jaribio lililotibuka la kumuua kaimu waziri wa ndani nchini Libya Al-Sidik Abdel-Karim. Shirika la kitaifa la habari LANA n...
-
Asema uchaguzi wa Urais uliopangwa kufanywa Mei 25, ni hatua inayofaa. Katika hatua ambayo haikutarajiwa Rais wa Urusi, Vladimir Putin, a...
-
Tanzania imesema inapambana na mlipuko wa homa ya dengue iliyozuka mapema mwaka huu. Watu watatu mpaka sasa wameripotiwa ...
-
Baadhi hutengeza maji ya sharubati kwa kuichanganya na matunda Baadhi wanaamini kuwa Kondo la nyuma huwa na madini mengi ambayo hayapaswi...
MITANDAO YA KIJAMII
TAFUTA HABARI ZILIZO SOMWA NYUMA
Pages
WALIO TEMBELEA
Powered by Blogger.
TANGAZA NASI
kwama Matangazo wasiliana nasi kupitia anuani zifuataz
Email:
mohamedwaziri295@gmail.com
mohamedwaziri21@yahoo.com
contact us:
0762118805
0658118804
info@islamicnews.blogspot.com
Wote mnakalibishwa
Email:
mohamedwaziri295@gmail.com
mohamedwaziri21@yahoo.com
contact us:
0762118805
0658118804
info@islamicnews.blogspot.com
Wote mnakalibishwa
Total Pageviews
Labels
DOWNLOAD QASWIDA
islamic
islami news
Social Icons
islamic
Blog Archive
Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...