Waziri wa mambo ya nje wa Syria, Walid Muallem, ametoa tisho la
kujiondoa kwenye mazungumzo ikiwa hakuna hatua zitakazokuwa zimefikiwa
Jumamosi
Mamilioni ya watu wameachwa bila makao kutokana na vita nchini Syria
Waakilishi wa serikali ya Syria katika mazungumzo ya amani kati ya
wanaharakati na serikali, wametishia kuondoka kwenye mazungumzo hayo ya
amani ikiwa mazungumzo muhimu hayatakuwa yameanza ifikapo Jumamosi.
Waziri wa mambo ya nje wa Syria, Walid Muallem, ametoa tisho la
kujiondoa kwenye mazungumzo baada ya kukutana na mjumbe maalum wa UN
nchini Syria Lakhdar Brahimi.
Bwana Brahimi anatarajiwa kukutana na upande wa upinzani baadaye Ijumaa.
Duru zinasema kuwa mazungumzo yamekumbwa na changamoto hasa kwa kuwa pande zote mbili zina misimamo mikali.
Mgogoro wa kisiasa nchini Syria, umesababisha vifo vya watu 100,000 kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.
Ghasia hizo pia zimesababisha watu milioni 9.5
kutoroka makwao, na kusababisha hali mbaya ya kibinadamu ndani ya Syria
na katika nchi jirani.
Hii ni siku ya tatu ya mazungumzo mjini Geneva lakini mkutano wa kwanza rasmi ambapo mazungumzo yanaanza.
Kulikuwa na matumaini ya mkutano wa ana kwa ana
kati ya serikali na wanaharakati, lakini baadaye bwana Brahimi alifanya
mazungumzo na kila upande.
Pande hizo zinalaumiana kwa changamoto hiyo.
Friday, 24 January 2014
Browse: Home
» Syria yatishia kujiondoa Geneva
Syria yatishia kujiondoa Geneva
Posted by mkachu |  Tagged as:
Habari na U Chambuzi
HALI YA HEWA
TANGAZANASI
MTANDAO WA KIJAMII
ZILIZO SOMWA ZAIDI
-
Chama Cha Mapinduzi (CCM) party stalwart Rostam Aziz has earned USD 240 million (about Tsh. 384,000,000,000/-) from selling part of his st...
-
eshi la Marekani limefanya shambulizi la makombora dhidi ya mtu anayeshukiwa kuwa mmoja wa viongozi wa al-Shabaab nchini Somalia. ...
-
Wanaume wengi wanapofikia hatua ya kuoa si kwamba wanakurupuka tu na kuoa mwanamke yeyote mwenye sura nzuri, bali huchukua muda wao mw...
-
Baadhi ya wanawake wengi wa hapa mjini wameanza kutumia style mpya ya kugundisha nywele aka wiving katika vichwa vyao kwa kutumia gu...
-
683 wahukumiwa kifo nchini Misri. ...
-
Maelfu ya watu wanaokabiliwa na uhaba wa chakula nchini Kenya wanatarajiwa kupata afueni baada ya Rais Uhuru Kenyatta kuzindua rasmi m...
-
Kumekuwa na jaribio lililotibuka la kumuua kaimu waziri wa ndani nchini Libya Al-Sidik Abdel-Karim. Shirika la kitaifa la habari LANA n...
-
Asema uchaguzi wa Urais uliopangwa kufanywa Mei 25, ni hatua inayofaa. Katika hatua ambayo haikutarajiwa Rais wa Urusi, Vladimir Putin, a...
-
Tanzania imesema inapambana na mlipuko wa homa ya dengue iliyozuka mapema mwaka huu. Watu watatu mpaka sasa wameripotiwa ...
-
Baadhi hutengeza maji ya sharubati kwa kuichanganya na matunda Baadhi wanaamini kuwa Kondo la nyuma huwa na madini mengi ambayo hayapaswi...
MITANDAO YA KIJAMII
TAFUTA HABARI ZILIZO SOMWA NYUMA
Pages
WALIO TEMBELEA
Powered by Blogger.
TANGAZA NASI
kwama Matangazo wasiliana nasi kupitia anuani zifuataz
Email:
mohamedwaziri295@gmail.com
mohamedwaziri21@yahoo.com
contact us:
0762118805
0658118804
info@islamicnews.blogspot.com
Wote mnakalibishwa
Email:
mohamedwaziri295@gmail.com
mohamedwaziri21@yahoo.com
contact us:
0762118805
0658118804
info@islamicnews.blogspot.com
Wote mnakalibishwa
Total Pageviews
Labels
DOWNLOAD QASWIDA
islamic
islami news
Social Icons
islamic
Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...